Jumapili , 27th Jan , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa wakuu wawili wa Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga na Mkuu wa Wilaya ya Tarime.

Mwenge Uhuru

Nafasi ya Mkuu wa wilaya ya Mwanga, ametauliwa Thomas Apson na Mkuu wa Wilaya ya Tarime ametauliwa ndugu Charles Kabeho.

Ndugu Charles Kabeho alikuwa kiongozi wa mwenge mwaka 2018 ambao ulizunguka nchi nzima kukagua na kuzindua miradi mbalimbali.

Pia Rais John Magufuli amewateua majaji 6 wa Mahakama Kuu, kuwa majaji wa Mahakama ya Rufani na mahakimu na wanasheria 15 kuwa majaji wa Mahakama Kuu.

Wateuliwa wote wataapishwa Jumanne, 29 Januari, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Itazame listi kamili ya wateuliwa hapa chini.