Nape Nnauye
Nkana ambayo ilichuana na Simba leo Jijini Dar es salaam kwenye Uwanja wa Taifa ilishuhudia Simba ikifanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano klabu bingwa Afrika kwa ushindi wa mabao 3-1.
Kupitia ukurasa wake Twitter Nape Nnauye ameandika ameshindwa kujiuzuia moja ya goli lilifungwa na mshambuliaji Clatous Chama na kusema bao hilo ni la aina yake.
"Nimejificha vya kutosha, lakini kwa goli hili, Simba hii kiboko This is Simba" aliandika Nape.
Watu wengine mashuhuri wakiwemo mastaa wa filamu na muziki wameelezea furaha zao juu ya ushindi wa Simba kama inavyoonekana hapo chini.
Basi ndugu wapambe nuksi,ndio kama mlivosikia.. pic.twitter.com/OdbQxiguJ8
— ChoirMaster... (@MwanaFA) December 23, 2018
Engineer Somaaaaa, Ngapi hizo???
Hongera Simba, Hongera Tanzania. Ni heshima kwa Nchi yetu na Soka letu. pic.twitter.com/0w6hMmLOWI— Dr.Mwigulu Nchemba (MG) (@mwigulunchemba1) December 23, 2018
binadam wabaya sana wameenda kabisa taifa kushangilia team nyingine halafu wameondoka wanaangalia ubao wa matokeo hawaamini
Mnyamaaaaaaa— Mwasiti (@mwasitij) December 23, 2018