Jumanne , 18th Dec , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Mh. Benjamini Mkapa kufuatia kifo cha Makamu wa chuo hicho Prof. Egid Beatus Mubofu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Kupitia taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu Gerson Msigwa imesema kuwa Rais Magufuli amemuomba Mkapa kufikisha salam zake za pole kwa familia ya marehemu Prof. Mubofu, wahadhiri na wafanyakazi, pamoja na wanafunzi wa UDOM.

"Nimesikitishwa sana na kifo cha Prof. Mubofu, nitamkumbuka kwa uchapakazi wake, ubunifu, uadilifu na uaminifu mkubwa aliouonesha katuika utumishi wake kwa Taifa ikiwemo kazi nzuri aliyojifanya katika shirika la viwango Tanzania (TBS), akiwa Mkurugenzi Mkuu kabla ya kuteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDOM" ,amesema Rais Magufuli

Marehemu, Prof. Mubofu enzi za uhai wake.

Prof. Mubofu amefariki dunia leo Disemba, 18 akiwa jijini Pretoria nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu zaidi, akitokea Taasisi ya Tiba ya Mifupa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI), alikokuwa akipatiwa matibabu ya Kiharusi.