Alhamisi , 7th Aug , 2014

Rapa Izzo Business, ameweka wazi sababu za kuendelea kufanya kazi zake za video za muziki na muongoza video Nick Dizzo kutoka E Media pekee, katika historia ya video za muziki ambazo huwa anazifanya.

rapa wa nchini Tanzania Izzo Bizness

Izzo ambaye wikiendi hii atakuwa katika jukwaa la Kili Tour Mbeya, amesema kuwa, Nick Dizzo ambaye atafanya naye video ya Walala hoi mwezi huu, ana uwezo mkubwa na mara nyingi sababu kubwa inayoficha uwezo wake ni ufinyu wa bajeti za kufanya video zenyewe.

Izzo Business amekuwa karibu sana na Nick Dizzo kutokana na jinsi muongoza video huyo naye kuwa mshabiki mkubwa wa nyimbo za rapa huyo maarufu nchini.