Alhamisi , 8th Nov , 2018

Idara ya uhamiaji nchini imesema haina lengo la kuwabagua wakazi wa Mkoa wa Kigoma pamoja na wakazi wengine wa maeneo ya mipakani bali walichokidai inalenga kuboresha hali ya ulinzi na usalama na kwenye maeneo hayo.

Msemaji Idara ya Uhamiaji Ally Mtanda, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe.

Ally Mtanda ambaye ni Mratibu wa Polisi Idara ya Uhamiaji nchini ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv ikiwa ni siku chache baada ya kutoa taarifa ya kuedelea kuchunguza uraia wa Abdul Nondo pamoja na Askofu Zakaria Kakobe.

si kweli lengo la idara ya uhamiaji kuwabagua watu wanatokea Kigoma, kila mahali kuna historia yake, mkoa wa Kigoma ina kambi zaidi ya tatu za wakimbizi kwa hiyo kuna muingiliano wa wahamiaji haramu ndio maana tunafanya ukaguzi ili kuwalinda watanzania wasipate madhara.”

Lengo letu si kuleta ubaguzi, suala la kiuchunguzi linapotokea mtu yeyote anaweza akatuhumiwa ili idara ya uhamiaji iweze kujiridhisha, wapo tuliowatuhumu hawatokei kwenye maeneo hayo, kimsingi sisi tunafanya kazi kwa usawa,” amesema Mtanda.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Zitto Kabwe akiwa bungeni alitoa madai juu ya kile alichokidai kuwa ni kubaguliwa kwa wakazi wa Kigoma ambao ni miongoni mwa mikoa ya mpakani.