
Mbunge, Suzan Lyimo na Rais John Magufuli
Akiuliza swali hilo kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Suzan Lyimo alidai anapata mkanganyiko afutae kauli ipi kati ya kauli ya Rais Magufuli au sera ya uzazi wa mpango.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri, Dkt Faustine Ndugulile amesema serikali haijatoa tamko la kusitisha huduma ya uzazi wa mpango bali Rais Magufuli alitaka watu wazae kulingana na uwezo wao.
“Sisi kama serikali hatujaweka ukomo wa idadi ya watoto wa kuzaa, tunachosema kama serikali, mtu awe na idadi ya watoto anaoweza kuwatunza, na hatujatoa na halitakuwepo tamko la kusitisha uzazi wa mpango, alichosema Rais mtu anakuwa na idadi ya watoto ambao ataweza kuwatunza.”
Agosti 12 mwaka 2016 akiwa Jijini Dar es salaam Rais Magufuli alisema “darasa la kwanza kwa mwaka huu wamefika milioni 2, nataka niwaeleze watani wangu wa Dar es salaam ni kuzaa tu, msihangaike kula dawa za majira, fyatua mtoto wako atasoma bure la kwanza mpaka sekondari.”