
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola
Waziri Lugola ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari nchini kufuatia kuwepo kwa kampeni maalum iliyotangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda juu ya kuanza zoezi la kuwakamata watu hao katika mkoa wake.
Kangi amesema “ninachosema kuwa ni Tanzania ni salama hakuna mtu yeyote anayeweza kusema kuwa sio salama bila ya kuwa na vigezo husika kama mtu yeyote anahatarishiwa maisha yake basi aende polisi na mimi sijapata taarifa zozote kutoka polisi zinazoeleza kuwapo kwa mazingira hatarishi ya watu hao", amesema Kangi.
Mapema wiki hii ubalozi wa Marekani nchini ulitoa onyo kali kwa raia wake waishio nchini kuwa makini na zoezi la kuwakamata watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Siku chache baada ya taarifa hiyo, serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga imesema msimamo uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ulikuwa ni msimamo wake binafsi na si wa serikali.