Jumatano , 6th Aug , 2014

Kilimanjaro Music Tour 2014, inarejesha mashambulizi yake nngwe ya pili kwa kishindo ambapo kazi inaanzia Mbeya katika ukumbi wa New City Pub Jumamosi hii.

Kili Music Tour 2014

Jukwaa litatikiswa na mastaa wanaotikisa game ya muziki Bongo akiwepo Shilole, Chibwa, Rich Mavoko, AY, MwanaFA, Professor jay, Weusi pamoja na mtoto wa nyumbani Izzo Business.

Kama kawaida, milango itafunguliwa saa 10 jioni, na kiingilio katika show hii ni shilingi 3,000 tu, ambapo mlangoni unazawadiwa kinywaji kimoja buree.

Hii si ya kukosa hata kidogo.