
Moja ya mchezo kati ya Gor Mahia na Simba
Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Goodson Park, ambapo Gor Mahia iliwasili nchini Uingereza Ijumaa ya wiki iliyopita.
Baada ya kuwasili nchini humo, Gor Mahia iliwashuhudia wapinzani wake Everton wakicheza mchezo wa EPL dhidi ya Brighton & Hove Albion, wikiendi iliyopita ambapo Everton iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Mchezo huo ni katika muendelezo wa mashindano ya Sporti Pesa yaliyofanyika mwanzoni mwa mwezi Agosti yakihusisha vilabu kadhaa vya Afrika Mashariki ili kumpata mshindi mmoja atakayekutana na Everton.
Mashindano hayo yalihusisha pia timu vigogo hapa nchini, Simba na Yanga ambazo hazikufanikiwa kufanya vizuri baada ya Yanga kutolewa katika hatua ya awali huku Simba ikitolewa katika hatua ya fainali na Gor Mahia ambayo sasa inapata nafasi ya kucheza na Everton katika miaka miwili mfululizo.