Wachezaji wa Mchenga Bball Stars (kijani) na Flying Dribblers (nyeupe).
Mchenga walianza mchezo huo kwa kasi wakishinda quarter ya kwanza kwa pointi 27 dhidi ya 10 za Flying Dribblers kabla ya kuendelea kuongoza kwa pointi 62 kwa 25 hivyo kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa tofauti ya pointi 37. Katika quarter hizo mbili mchezaji Baraka Sadick alifunga pointi 32.
Baada ya mapumziko Mchenga walirejea kwa kasi tena na kuongoza kwa pointi 62 dhidi ya 44 za Flying Dribblers. Mabingwa hao watetezi waliendelea na moto wao katika quarter ya 4 na kufanikiwa kufikisha pointi 100 ambapo hadi mwisho wa mchezo wakaongoza kwa pointi 103 kwa 73.
Katika mchezo huo mchezaji Baraka Sadick wa Mchenga Bball Stars ameibuka kinara wa jumla kwa kufunga pointi 48, Assist 6 na kuchukua rebound 4. Amefuatiwa na mchezaji Baraka Mopele wa Flying Dribblers ambaye amefunga pointi 29 na rebound 4.
Game 2 ya michuano hiyo inayodhaminiwa na kinywaji cha Sprite, itachezwa Jumatano Agosti 22, 2018 kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay. Mechi hizi zinaweza kwenda hadi game 5 endapo Flying Dribblers watarejea na kusawazisha katika game 2 na zinazofuata.