
Spray ambayo huyeyuka ndani ya dakika moja inavyotumika katika
mchezo wa Soka
Mvumbuzi huyo raia wa Brazil, Heine Allemagne mwenye miaka 47 amesema alivumbua teknolojia hiyo mwaka 2000 akiwa bafuni kwake kwa kutumia sabuni ya kunyolea ndevu na kuiendeleza mwenyewe kwa kutumia pesa yake kwa miaka 14 kabla ya kuionesha kwa maafisa wa FIFA ambao walirasmisha katika kombe la Dunia lililofanyika nchini Brazil mwaka 2014.
Baada ya kukaa na maafisa waandamizi wa FIFA akiwemo Rais wa zamani wa Shirikisho hilo Sepp Blatter walikubaliana kuwa FIFA ingenunua teknolojia hiyo kwa Pauni million 30 na kumfanya Allemagne kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa nchini Brazil.
Miezi michache baadae baada ya makubaliano hayo, FIFA ilimsaliti na kuanza kuyatafuta makampuni mengine kwaajili ya kuwapa teknolojia hiyo ili iweze kutengenezewa kwaajili ya majaribio katika mashindano yanayofuata.
“Nilihisi kuwa ndoto niliyokuwa naiota katika maisha yangu imetimia na maisha yangu yanakwenda kubadilika, kuwa nimeipandisha teknolojia yangu kuwa kubwa Duniani lakini sasa matumaini yote yameondoka . ninapoitazama teknolojia yangu inatumika katika soka sijihisi tena ufahari bali najihisi kuwa mtu nisiye na chochote", amesema Allemagne.
Heine Allemagne akiwa na gwiji wa soka wa Ufaransa, Michel Platini katika picha ya pamoja kwenya makao makuu ya FIFA, picha ya pembeni inamuonesha Heine Allemagne akiwa na kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.
FIFA wamekana kuzungumzia chochote kuhusu tuhuma hizo huku Heine Allemagne na wakili wake wakiamini kuwa iko siku haki yao itapatikana na hatimaye kuwekwa katika historia kubwa ya wavumbuzi wa teknolojia nzuri inayosaidia katika soka Duniani .
Teknolojia hiyo ilianza kutumika katika soka kwa mara ya kwanza mwezi june mwaka 2014 katika kombe la Dunia katika mchezo wa Ufunguzi kati ya Brazil na Croatia na baadae kusambaa duniani kote zikiwemo ligi kubwa mbalimbali barani Ulaya kama Premier League, Laliga, na Serie A.
Source: Daily Mail