Meneja wa mchezaji huyo Suleiman Haroub amesema kwamba hadi sasa amepokea ofa nne zikiwemo za timu za JKT Tanzania na KMC ambazo zote zitashiriki ligi kuu msimu ujao.
Kakolanya amekosa namba mbele ya walinda milango Youthe Rostand na Ramadhani Kabwili huku pia mkataba wake ukiwa unaelekea kumalizika hivyo meneja wake amesisitiza kuwa bado wanaisikiliza Yanga kabla ya kutazama ofa nyingine.
"Ni kweli hizo ofa zipo tumezipokea na wamekuja tumezungumza nao lakini bado tunawasikiliza Yanga ambao hadi sasa wanamkataba naye lakini wapo kimya'', amesema Haroub.
Golikipa huyo kwasasa kaachwa nchini na kikosi cha Yanga kilichosafiri kwenda Botswana kwaajili ya mchezo wa marudiano ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers. Mchezo huo utapigwa kesho jioni na katika mchezo wa kwanza Township ilishinda 2-1.