Jumanne , 1st Jul , 2014

Serikali na wadau mbalimbali wa michezo nchini Tanzania wametakiwa kujitokeza na kuudhamini mchezo wa kuogelea ambao umeonekana kutopewa kipaombele licha ya kuwepo kwa wachezaji na makocha wazuri wa mchezo huo hapa nchini.

Akizungumza na Muhtasari wa michezo leo, wakati wa kufunga mafunzo ya kuogelea kwa waalimu, Mkurugenzi wa Chama cha Kuogelea ambaye pia ni mratibu wa mafunzo hayo Marcelino Ngalioma amesema mchezo wa kuogelea umesahaulika na hivyo kuna haja sasa watanzania na serikali kwa ujumla wakaongeza nguvu katika udhamini.

Nao Makocha waliohitimu Kozi wapatao 22 miongoni mwao wamesema mafunzo hayo watayatumia katika kuwahamasisha vijana kushiriki zaidi katika mchezo wa kuogelea.

Kozi hiyo imeendeshwa na mkufunzi kutoka chama cha kuogelea duniani (FINA) Matthias Ludwing.