Jumamosi , 10th Feb , 2018

Msanii ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya 'amezoea' amefunguka na kudai sifa pekee anazoziangalia pindi anapochagua mwanaume wa kuwa nae katika mahusiano yake ni lazima awe ana mjali yeye zaidi kuliko maisha yake.

Lulu amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza katika 'Backstage' ya Bongo flava Top 20 kutoka East Afrika Radio baada ya kuulizwa ni kigezo gani huwa anaangalia pindi anapotaka kuwa na mwanaume katika mahusiano yake.

"Nampenda mwanaume ambae ananijali, anamkumbuka Mungu halafu anaweka maisha yangu kwanza kuliko ya kwake binafsi, awe ananisikiliza pamoja na kujali familia yake kwa sababu mtu anayeweza kujali familia yake inakuwa rahisi hata kujali ya kwangu", amesema Lulu.

Kwa upande mwingine, Lulu Diva amewashakuru mashabiki zake kwa kuipokea vizuri wimbo wake wa amezoea ambao alitoa mwisho wa mwezi Januari.