Akichat na wadau wa burudani live kwenye #KIKAANGONI kupitia facebook page ya East Africa Television, Idris amesema Beyonce ni mwanamke mwenye sifa thabiti za kuwa mwenza, hivyo hata yeye mpenzi wake ajaye lazima awe na sifa kama za Beyonce.
“Mwanamke ambaye mi nataka nije kutoka naye, anatakiwa awe kama Beyonce kiukweli, factors zake ni kwamba anajielewa, ana msimamo, ni mzuri ndani na nje, tabia yake, ni mchapakazi sana, very challenging, ikitokea sasa hivi Jayz akamuacha Beyonce, Beyonce hataathirika katika kazi zake, hata hivyo ana hela uliko Jay Z, ni independent, mi nahitaji mwanamke ambaye anaweza akawa challenge kwangu”, amesema Idris Sultan.
Hivi karibuni muigizaji huyo amekuwa akitengeneza picha kuonekana yuko na Beyonce, picha ambazo amedai Jay Z kamtumia ujumbe kuwa hajafurahishwa nazo.
Kikaangoni imedhaminiwa na Vodacom, PESA NI M-PESA, Lipa sasa kwa M-PESA upate punguzo la vitu mbali mbali



