Jumapili , 29th Jun , 2014

Msanii nyota wa nchini Nigeria David Adedeji Adeleke aka Davido tayari amekula shavu la kutumbuiza katika sherehe za siku ya ukombozi ambazo zitafanyika tarehe 4 mwezi July mwaka huu katika uwanja wa taifa wa Amahoro nchini Rwanda.

Msanii Davido wa nchini Nigeria

Davido atakuwa akitumbuiza katika tamasha hilo sambamba na wasanii maarufu wa nchini humo wakiwemo Jay Polly, Dream Boys, Urban Boyz, na wengineo wengi.

Aidha mwanadada Cinderella Sanyu aka Cindy wa nchini Uganda atakuwepo kuiwakilisha nchi yake katika sherehe hizo za miaka 20 ya ukombozi wa nchini Rwanda.