Jumamosi , 21st Jun , 2014

Leo hii patakuwa hapatoshi pale Iringa ambapo kuanzia muda huu ile ziara gumzo ya muziki, aka Kili Music Tour 2014 ipo tayari kabisa kwaajili ya bonge moja la shoo kutoka kwa wasanii wakali wanaotamba kwa sasa nchini Tanzania.

Biashara yote ni pale katika uwanja wa Samora ambapo jukwaani ni mashambulizi kutoka kwa wakali wa Muziki Mwana FA , Professa Jay, Linex, Mwasiti, Izzo Business, Snura, AY, Richa Mavocal pamoja na Weusi, yani ni moto juu ya moto hii si ya kukosa kabisa.

Timu nzima ya East Africa Radio na East Africa Television tayati kwa kukuendeshea mchongo mzima, hapa Mjukuu wa Ambua Dullah, huku Sam Misago na katika 1 na mbili ni DJ Mafuvu.

Iringa yote tunatimba pale, Tunazungusha Kwetu Kwetu.