Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Afande Sele amesema mama Kanumba ni mama ambaye hana vigezo vya kuwa mzazi kwani hana uchungu na mtoto wa mwenzake kwenda jela akiwa mdogo, huku ambaye alistahili kuhukumiwa ni mtoto wake Kanumba.
"Mama Kanumba nimeshangaa kusikia anashukuru kwamba Lulu kafungwa, mama ambaye hana uchungu hana sifa ya kuwa mzazi, anashukuru kwamba mtoto mdogo anafungwa kwa ajili ya ubazazi wa mtoto wake, ujinga wa mwanae, upuuzi wa mwanae, mkubwa anambaka mtoto mdogo kama yule”, amesema Afande Sele.
Afande Sele ameendelea kwa kusema kwamba yeye kama mzazi mwenye mtoto wa kike anatamani hata maiti ya Kanumba ingefukuliwa ichomwe mto ili kuwa fundisho kwa wanaume wengine wenye matendo kama yake.