Miss Tanga 2014
Shindano la kumsaka mrembo huyu wa jiji la Tanga, litafanyika tarehe 21 mwezi huu Tanga Beach Resort kuanzia saa 1 usiku, katika tukio litakalopambwa na burudani mbalimbali ikiwepo show ya aina yake kutoka kwa Malkia wa Mipasho, Bi Khadija Omar Kopa.
Tiketi kwa ajili ya tukio hili zitaanza kupatikana Alhamisi tarehe 19 mpaka tarehe 21 mwezi huu katika hoteli ya Tanga Beach Resort na Mkonge Hotel kwa gharama ya shilingi 10,000 kwa viti vya kawaida na 30,000 kwa VIP pamoja na vinjwaji.
Kumbuka, Mshindi wa shindano hili ataondoka na zawadi nono ya Gari aina ya Vitz.
Weka hii katika ratiba yako na ujipange kutokukosa Miss Tanga 2014.