Baadhi ya wakazi wa Babati wakiwa wamezuia msafara wa Abdulrahman Kinana katibu mkuu wa CCM
Watu wa jamii za kifugaji katika halmashauri ya Babati vijijini wamelazimika kuzuia kwa muda msafara wa katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ili asikie kero yao ya kudhulumiwa ardhi yao na mwekezaji kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji vya Vilima vitatu, Mausaa na Nkaiti
Wakizungumzia kero hiyo wakazi hao wamesema viongozi wa serikali za vijiji hivyo wamegawa eneo bila kuwahusisha na sasa wanafukuzwa na nyumba zao kuchomwa moto bila kuoneshwa mahali mbadala huku wakazi wa kijiji cha Galapo nao wakilalamikia kuongezwa kwa mipaka ya hifadhi na kuingia katika eneo la kijiji.
Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ameonesha kuchukizwa na ongezeko la migogoro ya ardhi na kuongeza kuwa hali hiyo inatokana na watendaji kutoshughulikia kwa wakati matatizo ya wananchi na kuahidi kulishughulikia suala ilo.