Alhamisi , 29th Mei , 2014

Uongozi wa Yanga umewataka wanachama wao kujitokeza katika mkutano mkuu wa klabu hiyo huku ukitoa onyo kwa wanachama ambao hawajalipia kadi kuwa watakosa haki ya kushirki katika mkutano huo

Umati wa wanachama wa klabu ya soka ya Yanga wakiwa katika moja ya mikutano ya klabu hiyo.

Mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba ya klabu ya soka ya Dar es salaam Yanga unataraji kufanyika Juni mosi mwaka huu katika ukumbi wa bwalo la maofisa wa polisi Oysterbay jijini Dar es salam.

Afisa habari wa Yanga Baraka Kizuguto amesema kuwa ajenda za mkutano huo utakaoanza saa 3 asubuhi ni kufanya marekebisho ya katiba kwa kuzingatia maelekezo ya TFF.

Aidha Kizuguto amesema wenye haki ya kuhudhuria mkutano huo muhimu ambao ndio utatoa picha ya mwelekeo wa kuelekea uchaguzi wa klabu hiyo ni wanachama wa klabu hiyo ambao wako hai akimaanisha wale wote ambao kadi za uanachama wao zimelipiwa mpaka kipindi cha kufanyika mkutano huo.