
Hayo yamesemwa na Kocha na mkufunzi wa kimataifa wa mchezo wa mpira wa kikapu na mratibu wa Junior NBA, Bahati Mgunda kuwa ujio wa ligi hiyo umewapa fursa vijana katika kuonesha vipaji walivyo kuwa navyo.
"Ligi hii mpya iliyoanzishwa na EATV LTD, kushirikiana na Sprite itabadilisha sana muonekano wa mpira wa kikapu pia itatoa 'challenge' kwa viongozi au timu zinazoshiriki ligi iliyopo juu ya RBA kwa kutoa zawadi kubwa kwa bingwa" - alisema Mgunda
Siku ya Jumamosi katika hatua ya mtoano wa kutafuta timu 16 bora utafanyika katika viwanja vya JK Park, kidongo chekundu, Kariakoo Jijini Dar es salaam, Mtifuano huo utazikutanisha timu 52 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi zilizoweza kufuzu hatua za awali za usahili wa kugombea kitita cha fedha taslimu Milioni 15 katika mashindano hayo,