Pallaso amesema kuwa ni kweli ugomvi ulikuwepo lakini haukuhusisha mapigano yoyote yale kati yake na Radio.
Pallaso amesema kuwa, siku ya tukio ni kweli kulizuka purukushani ya maneno kulikozua ugomvi kwenye moja ya baa uliotokana na bifu lililopo kati ya kundi la Goodlyfe na mahasimu wao "Team No Sleep" ambalo limeibuka baada ya mpasuko.
Pallaso kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema kuwa, Radio ni kaka yake na taaarifa za yeye kupigana na Radio zimetengenezwa kwa lengo la kumchafulia jina tu.