Ijumaa , 12th Mei , 2017

Baada ya kupotea kwa wiki mbili mrembo wa Afrika Kusini, Karabo Mokoena amekutwa amefariki dunia huku taarifa za awali zikidai kwamba ameuawa na mpenzi wake wa zamani.

Baba mzazi wa marehemu kupitia mtandao wa Facebook ametoa taarifa mwanaye amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa umechomwa moto na kwamba muuaji wa tukio hilo bado anasakwa na polisi.

“The boyfriend has confesses, He killed and burned my daughter,” ameandika Tshepo (baba wa marehemu Karabo)kwenye mtandao huo.

Ujumbe wa Facebook wa Mzazi wa Karabo.

Habari za kupotea kwa binti huyo zilianza kusambaa mitandaoni kuwa anatafutwa kutokana na kupotea kwake tangu April 28, huku rafiki yake Karabo wa karibu  'Stephanie Leong' akiomba misaada kwa watu mbali mbali waliomuona Karabo wampatie taarifa