Jumatano , 10th Mei , 2017

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam zimesababisha vifo vya watu wawili na kuleta maafa na uharibifu mali na miondombinu.

Akiongea na wanahabari Jijini Dar es Salaam leo, Kamishna Sirro amesema kifo cha kwanza kimetokea eneo la Goran Suka ambapo Alice Genadi alitumbukia kwenye shimo la choo cha nyumba ya jirani ambacho kilikuwa kimejaa na wa pili ni Laimu Zakaria Mkazi wa Kimara Temboni ambaye ni fundi ujenzi ambaye alidondokewa na ukuta ambao alikuwa alikuwa akiubomoa.

Kamanda Sirro pia amesema maeneo ya Golani Kimbiji ulitokea upepo mkali ambao uling'oa miti na mapaa ya nyumba 6 na waanga wa tukio hilo wamepatiwa misaada ya kibinadamu kusababisha uharibifu wa barabara maeneo ya Mwasonga na kusababisha malori zaidi ya 20 kukwama katika barabara hiyo.

Mtazame hapa Kamishna Sirro akielezea tuko hilo,