Daniel Wanjiru kutoka Kenya aliibuka kinara wa mbio hizo akitumia muda wa saa 02:05:48, nafasi ya pili ikichukuliwa na Kenenisa Bekele wa Ethiopia aliyetumia muda wa saa 02:05:57.
Nafasi ya tatu ya mbio hizo imeenda kwa mkenya mwingine Bedan Karoki aliyetumia muda wa saa 02:07:41, nafasi ya nne ikaenda kwa mkenya Abel Kirui akitumia muda wa saa 02:07:45, na namba tano ikienda kwa mtanzania Alphonce Simbu aliyetumia muda wa saa 02:09:10.
Timu ya East Africa TV & Radio inapenda kutoa pongezi kwa Alphonce Simbu kwa hatua aliyofikia.