Jumamosi , 25th Mar , 2017

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha mapinduzi , Humphrey Polepole amesema hadi kufikia jana Machi 24, wanachama wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge wa Afrika Mashariki walikuwa 452.

Basila Mwanukuzi na Seki Kasuga

 Karibu wa Itikadi na Uenezi CCM- Humphrey Polepole

Katika zoezi hilo la kuchukua fomu vijana wengi wa CCM wameonekana kuchangamkia nafasi hiyo ya ubunge wa EALA akiwemo aliyekuwa miss Tanzania wa zamani Basila Mwanukuzi,  kada mkereketwa Seki Boniventure Kasuga na wengine wengi.

Huu ni mchakato wa ndani wa chama hicho ili kupata wawakilishi na Ndugu Humphrey Polepole amesisitiza uadilifu.

"Tumesisitiza tena rushwa na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na kanuni za uchaguzi na uongozi havitavumiliwa, wote watakaoshiriki matendo hayo vikao vya chama vitayaondoa majina yao". Alisema Polepole
 

Seki Kasuga

Chama cha CCM kinatakiwa kutoa wawakilishi 6 watakaokwenda kuwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika (EALA)

Basilisa  Mwanukuzi akiwa ametoka kuchukua fomu