Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo mara baada ya kumuapisha Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Ametoa wito kwa uongozi mpya wa Jeshi hilo chini ya Jenerali Venance Mabeyo kuendeleza juhudi za kuilinda nchi na kuhakikisha viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya majeshi kama vile sare na vifaa, vinajengwa.
Rais Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange kwa kuliongoza jeshi hilo kwa kipindi chote alichokuwa madarakani na kueleza kuwa watanzania wana imani kubwa na JWTZ.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali James Mwakibolwa kuwa mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kuapishwa kushika wadhifa wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Rais Magufuli amemvalisha Jenerali Venance Salvatory Mabeyo cheo kipya cha Jenerali alichopandishwa kutoka Luteni Jenerali.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance Salvatory Mabeyo ambaye sasa ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Jenerali Juma Malewa kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Kamishna Juma Ali Malewa kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza.
Kabla ya kuapishwa kushika wadhifa huo, Mhe. Rais Magufuli amevalisha Kamishna Juma Ali Malewa cheo kipya cha Kamishna Jenerali.
Kamishna Jenerali Juma Ali Malewa amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna John Casmir Minja ambaye amestaafu.
Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Balozi. Luteni Jenerali Mstaafu Paul Meela kuwa Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mhe. Balozi Luteni Jenerali Mstaafu Paul Meela anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Antony Ngereza Cheche ambaye amestaafu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Paul Meela kuwa Balozi nchini DRC Congo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Pia, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Balozi Samuel Shelukindo kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa.
Mhe. Balozi Samuel Shelukindo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Balozi Begum Taj ambaye amestaafu.
Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Bw. Nyakimura Mathias Muhoji kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma.
Bw. Nyakimura Mathias Muhoji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Claudia Mpangala ambaye amestaafu.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia tukio la kuapishwa kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kamishna Robert Boazi Mikomangwa.
Kamishna Robert Boaz Mikomangwa ameapishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi - Ernest Mangu.
hafla hiyo imehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Kaimu Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
Tazama video.......