Jumatatu , 19th Mei , 2014

Msanii wa muziki Kala Jeremiah, amesema kuwa, licha ya soko la albam za muziki kusuasua hapa Bongo, kwa sasa soko la show lililoibuka ndio mkombozi wa wasanii na linalipa vizuri.

Kala Jeremiah amesema kuwa, pesa ambayo wasanii wanapata sasa kwa show ni nzuri ingawa bado kuna haja ya mashabiki kuongeza uzalendo, mapenzi na sapoti kwa kazi za wasanii kwa kuzinunua kazi halisi wanazotengeneza.

Kala Jeremiah amesema kuwa, kutokana na soko la muziki kugeuka namna hii, hatatoa tena albam mpaka ikipita kipindi cha miaka mitano kutoka sasa kwaajili ya mashabiki wake.