Jumatano , 21st Dec , 2016

Nigeria imekamata magunia 102 ya mchele wa plastiki yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sikukuu za krismas na mwaka mpya.

Maafisa nchini Nigeria baada ya kukamata mchele huo

Afisa wa forodha katika mji mkuu wa nchi hiyo , Lagos amesema Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' , baada ya kuuchemsha, na kuonekana kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida.

Hata hivyo amewaonya wahujumu wa uchumi ambao wanatumia kipindi hiki cha sikukuu kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu na kuwa watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mchele huo wa plastiki ulikua na nembo iliyoandikwa "Best Tomato Rice". Huku Uchunguzi ukiendelea ili kubaini kiwango cha mchele huo kimeuzwa mpaka sasa na jinsi ya kuondoa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha anza kuutumia.