Alhamisi , 15th Mei , 2014

Rapa mkali wa Kike, Witnesz ambaye kwa sasa ni mjamzito mwenye matarajio ya kuwa mama ndani ya miezi kadhaa ijayo, kupitia eNewz rasmi, ameweka wazi juu ya mahusiano yake na msanii Ochu Sheggy ambaye pia kwa sasa muda wote wanafanya muziki pamoja.

Witnesz na Ochu Sheggy - Ochuness

Witnesz amesema kuwa, mbali na mapenzi wakiwa kama wasanii wa muziki, yeye pamoja na baba mtarajiwa wa mtoto wake kwa pamoja wanatambulika kama 'Ochuness', wakiwa na mpango wa kuachia kazi mpya ambayo itawaeleza mashabiki mambo mengi kwa undani kuhusiana na mahusiano yao.

Kupitia mahojiano exclusive ambayo eNewz imefanya na wapendanao hawa, wamesema kuwa, hawana haraka na mpango wa kuhalalisha mahusiano yao katika kuingia katika ndoa, na wanafanya kila kitu taratibu kwa kuzingatia usemi wa mambo mazuri hayataki Haraka.