
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi akihojiwa na Waaandishi wa Habari.
Mkataba huo wa makubaliano ya kuendesha hospitali hiyo unasainiwa chini ya mkuu wa mkoa wa Njombe, kukiwa na wataalamu wa ofisi yake na mkurugenzi wa halmashauri ya Mji akiw ana wataalamu wake na mwenye halmashauri.
Mkataba huo unasainiwa ukiwa na lengo la kuboresha huduma za afya hospitalini hapo ambapo sasa bajeti yake itakuwa ya kimkoa na kuhudumia watu wa mkoa mzima tofauti na hapo kabla ilikuwa kuhudumia mkoa huku bajeti ikitolewa ki-halmashauri.
Baada ya kusaini mkataba huo ambao unasainiwa kwa muongozo wa mwanasheria wa mkoa wa Njombe Hilmar Danda mkuu wa mkoa Dkt. Rehema Nchimbi anasema kuwa sasa huduma itaboreshwa na changamoto zote zitatuliwa.