Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Dkt. Said Mawji imeeleza kuwa wagonjwa hao watatu wamelazwa katika kituo cha afya cha Lumuna na kufanya idadi kuongezeka tangu ugonjwa huo ulipoingia mkoani humo Oktoba 26 mwaka huu.
Watu wawili wameripotiwa kufariki ambao wote wanatokea wilaya za jirani, huku akitaja wilaya ambazo zimeathriwa na ugonjwa zikiwa ni pamoja na Dodoma mjini, Mpwapwa na Kongwa na kuwa wameandaa mikakati katika ngazi zote ili kutokomeza ugonjwa huo katika mkoa huo.