
Katika huduma hiyo vibali kutoka taasisi zote zinazohusika na uwekezaji nchini zitapatikana katika sehemu moja.
Waziri ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ndiye aliyefungua kituo hicho jijini Dar es Salaam leo ambapo katika maelezo yake amezitaka taasisi za umma kufanya kazi kwa ushirikiano ili kupunguza urasimu usio wa lazima na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara.
Awali akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw. Clifford Tandari amesema wao kama kioo cha wafanyabiashara wanaokuja kuwekeza nchini wamejipanga kuhakikisha kuwa huduma wanazotoa zinachochea ukuaji wa uchumi kama yalivyo matarajio ya serikali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Bw. Godfrey Simbeye ameipongeza hatua hiyo ya serikali na kwamba inaonesha matumaini ya kufikia uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni 25 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.