
Anna Mghwira - mwenyekiti ACT-Wazalendo
Amesema hali hiyo inatokana na kutozingatia baadhi ya madai muhimu ya wanawake.
Mghwira amesema kuwa miaka kumi iliyopita harakati za wanawake zilipiga hatua kubwa kwa kuwa serikali ilitekeleza suala hilo takribani asilimia 30 hususani uwakilishi katika nafasi za uongozi.
Amesema ajenda ya haki za wanawake inakosa nguvu kwa sasa kutokana na kukosa haki ya kikatiba kuhusu haki ya usawa wa kijinsia ambayo ilipendekezwa katika mchakato wa katiba mpya.
Aidha Mghwira asema licha ya kuwepo kwa jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli tangu alipoingia madarakani ikiwemo kurudisha nidhamu kwa watumishi wa umma bado harakati za kumkomboa mwanamke dhidi ya mfumo unaokandamiza haki na usawa zimesahaulika.