Kaimu Mkurugenzi WLAC - Rehema Msami
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake WLAC Rehema Msami alisema takwimu zilizoripotiwa mwaka jana zilionesha kuwa kesi za ukatili wa kingono zilikuwa 245.
Msami alisema matukio hayo yametokea katika wilaya ya Muleba, Kasulu, na Kinondoni hivyo juhudi za haraka zinahitajika ili waweze kutoa elimu kwa wananchi hali ambayo wanaamini inaweza kupunguza ukubwa wa tatizo.
Aliongeza kuwa licha ya kutokea kwa ukatili huo lakini pia kesi za ukatili jumla zimefikia 6,853 katika kipindi cha mwaka jana pekee.
Alisema kutokana na hali hiyo serikali inapaswa kushirikiana na wadau mbalimbali ili waweze kuangalia namna ya kupunguza vitendo vya ukatili.