Q Chillah ndani ya studio za EA Radio
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Q Chief amesema majukumu ya kazi zake za muziki ndiyo yalimfanya awe kimya kwenye suala la ndoa ambalo alishatangaza, lakini siku si nyingi atalirudia kwani yuko na binti ambaye anampenda sana na kwake ndiye "wife material".
“Niko na binti ambaye nampenda sana na katika kipindi chote hiki cha maumivu alikuwa na mimi, akijaribu kuni'encourage', anaelewa nini maana ya maisha, anajua nini kuanguka na kusimama tena, sema kazi za muziki ndizo zilinifanya nisitishe suala la ndoa, ila kwa sasa nadhani kila kitu kitaenda sawa, na kama unavyojua suala la ndoa ni makubaliano ya familia mbili yule ni mtoto wa watu”, alisema Q Chief.
Q Chief aliendelea kwa kumtaja mpenzi wake huyo anayejulikana kwa jina la Elizabeth kuwa ndiye mwanamke wake, na ndiye atakayefunga naye ndoa muda utakapofika.