Jumatano , 9th Nov , 2016

Wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe wanatarajia kutatua tatizo la upasuaji kwa mama wajawazito na upasuaji mwingine wa wagonjwa baada ya halmashauri hiyo kuanza kujenga chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Lupembe.

Mkuu wa mkoa wa (katikati) Dkt Rehema Nchimbi, kushoto ni mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri na wa kushoto ni mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessy.

Ujenzi huo unaenda sambamba na ujenzi wa wodi ya kulaza akinamama kituoni hapo ambapo awali wakazi wa halmashauri hiyo walikuwa wakitegemea hospitali ya halmashauri ya Mji Njombe ya Kibena ambayo ipo mbali na maeneo yao.

Akizungumzia juu ya ujenzi huo mganga mfawidhi wa kituo hicho Stanslaus Mwakiwia amesema kuwa asilimia 70 ya wagonjwa watatibiwa hapo baada ya kukamilika kwa jengo hilo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameomba jengo hilo kukamilika mapema ili kuokoa kina mama wengi wa mkoa huo pamoja na kupunguza vifo vya mama na mtoto.