Jumatano , 26th Oct , 2016

Kawhi Leonard, amefunga pointi 35, wakati akiisaidia San Antonio Spurs, kuifunga Golden State Warrors, kwa vikapu 129-100, usiku wa kuamkia leo, katika dimba la Oracle Arena, Oakland.

Kawhi Leonard, kushoto, akijaribu kuumiliki mpira wakati left, Stephen Curry naye akijaribu kumkaba

 

Akichezea kwa mara ya kwanza Golden State Warriors, Kevin Durant, alifunga pointi 27 na mipira iliyorudi 10, lakini mambo yalikuwa magumu, na hivyo timu yake hiyo mpya kupoteza mchezo huo.

Na katika mchezo mwingine mkubwa wa usiku wa kuamkia leo,  LeBron James aliwasaidia mabingwa watetezi wa NBA, Cleveland Cavaliers, kuifunga New York Knicks, kwa vikapu 118-88.