Jumanne , 13th Sep , 2016

East Africa Television LTD leo imezindua rasmi zoezi la kuchukua fomu za kushiriki EATV AWARDS, zinazotarajiwa kufanyika mwezi Desemba 2016.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Meneja Masoko wa EAV Ltd Roy Mbowe, amesema zoezi hilo litakuwa ni la siku 30, na litahusisha wasanii wote wa filamu na muziki, kama zinavyohitaji tuzo hizo.

"Leo tumekuja hapa kuzindua rasmi wasanii kuanza kujipendekeza kushiriki kwenye #EATV AWARDS, wasanii wanaji-nomanate wenyewe kwenye vipengele hivyo 10, na fomu zinaweza kujazwa na msanii mwenyewe au meneja wake, lakini pia lazima kuwe na mashahidi watakaojaza pia, kazi ambazo zitapokelewa ni zile ambazo zimetoka kuanzia tarehe 1 Julai 2015 mpaka tarehe 30 Juni 2016, hivyo msanii ukitaka kujipendekeza kuna sehemu mbili tu ya kupata fomu, nayo ni https://www.eatv.tv/awards na ofisi za EATV zilizopo Mikocheni DSM, na fomu zitakuwa 2, moja ni fomu ya kujipendekeza (nomination) na ya pili ni ya 'sheria na kanuni za ushiriki", alisema Roy Mbowe.

Roy Mbowe aliendelea kusema kuwa fomu hizo zikishachukuliwa na kujazwa, msanii atalazimika kuzirudisha kwenye ofisi za EATV akiambatanisha na kazi zake, ambazo amependekeza zishiriki kwenye tuzo.

"Utaratibu wa kuzirudisha unatakiwa uzilete studio pamoja na kazi yako, kwa wasanii wa muziki weka kwenye CD yako, wa filamu weka CD 2 tofauti na uzilete, Cd mbili kwa sababu ikitokea bahati mbaya moja isipocheza kazi zako, so moja itakuwepo, mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tar 12 Oktoba 2016 saa 11 jioni", alisema Bw. Mbowe.

Pia Bw. Mbowe aliendelea kwamba kwa msanii ambaye atahitaji maelekezo zaidi jinsi ya kujaza fomu hizo, anaweza akawasiliana na EATV kupitia barua pepe yake ambayo ni [email protected] au apige simu namba 0765885759, na tapewa maelekezo zaid.

Tags: