Jumatano , 7th Mei , 2014

Baada ya tuzo za muziki za Kilimanjaro kwa mwaka 2014 kumalizika mwisho wa wiki na washindi wa mwaka huu kufahamika, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe amesifia utaratibu na teknolojia iliyotumika katika zoezi la upigaji kura.

George amekanusha kuwepo kwa hujuma yoyote kutoka kwa wasanii na wadau katika kubadilisha ama kupanga matokeo.

Kavishe amewataka watu kutambua uhalali wa washindi wote huku akisema kuwa, zoezi zima la kura lilisimamiwa na kampuni nyingine na mchakato mzima kwa yeyote mwenye malalamiko upo wazi, ukiwa unaonyesha rekodi zote za wapiga kura na namba zao, kwa msanii yoyote atakayetaka kuona na kuhakikisha.