Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura
Maandalizi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kujipima uwezo baina ya wenyeji Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya timu ya taifa ya Malawi The flames mchezo utakaofanyika may 4 katika uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jijini Mbeya yamekamilika.
Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema kila kitu kiko sawa ikiwemo ujio wa Malawi ambao walitua nchini Hhapo jana usiku,
Wambura amesema mchezo huo pamoja na kuchezwa jijini mbeya kwa mara ya kwanza utafuata taratibu zote za kisheria za kimataifa za soka.
kwa upande mwingine Timu ya Taifa ya Malawi (Flames) imewasili jijini Mbeya tayari kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Mei 4 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.
Flames ikiwa na msafara wa watu 31 imewasili jana (Mei 1 mwaka huu) saa 1 jioni kwa njia ya barabara, na imefikia hoteli ya Manyanya. Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo jijini Mbeya tangu Aprili 27 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo.
Kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa sh. 5,000 wakati tiketi zitauzwa siku ya mchezo kuanzia saa 2 asubuhi katika vituo vya Uyole, Mwanjelwa,, Mbalizi, Stendi Kuu, Holiday Inn na Uwanja wa Sokoine.
Kwa mujibu wa TFF, Magari yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani ni ya wachezaji, gari la wagonjwa, gari la zimamoto na gari la waamuzi pekee.