Jumatano , 10th Aug , 2016

Meneja wa muziki wa bongo fleva anayefahamika kwa jina la Maneno ameliomba Baraza la Sanaa Tanzania BASATA kutoa elimu kwa wana muziki wa bongo fleva ili kuboresha kazi zao.

Maneno pia amelitaka baraza hilo liweke sheria pamoja na taratibu ambazo zitawaongoza wasanii ili wakiwa wanafanya kazi zao waweze kuzingatia taratibu hizo.

Ameendelea kuomba baraza hilo la sanaa lisisubiri tu kuona ni msanii gani kakosea kwenye kazi yake ili wamfungie au kulipa faini kwani hiyo ni chachu kwa wasanii hao na haliwajengi kimuziki kwani suluhisho ni kutoa elimu katika sekta zote za sanaa.