Alhamisi , 4th Aug , 2016

Hosiptali ya Taifa Muhimbili imewataka Watanzania kuhakikisha wanajiunga na bima ya Afya ili kuepuka garama kubwa za matibabu sambamba na kuipunguzia gharama kubwa hosptali hiyo yakutumia shilingi milioni 600 kuwahudumia wagonjwa wa msamaha.

Akiongea na EATV hosptalini hapo juu ya hatua ambazo hosptali hiyo inachukuwa kuhakikisha kuwa inatoa huduma bora kwa wote msemaji wa hosptali hiyo Bwana Aminieli Eligaesha amesema muhimbili inaingia garama kubwa ya kuhudumia wagonjwa wenye msamaha garama ambazo zingefidiwa na bima ya afya na kuwezesha uendeshwaji wa hosptali hiyo

“Bima ya afya inarahisisha upatikanaji wa huduma, pia itatuwezesha Muhimbili kupata kiasi Fulani cha mapato kutoka kwa kila mgonjwa nivyema wananchi wakajiunga na bima ya afya ili kuepuka garama kubwa za matibabu” amesema Eligaesha

Aligaesha amesema baada ya Hosptali hiyo kutatua kero ya matibabu kupitia mashine za MRI, XRAY na CT SCAN kwa sasa hosptali ya muhimbili imejipanga kuondokana na kero ya ucheleweshwaji wa huduma ambapo kuanzia september wagonjwa watalipia matibabu yao kwanjia ya kadi hali ambayo itaondoa upotevu wa fedha na kuboresha huduma

“Tunaanzisha malipo kwa njia ya kadi na malipo kwa njia ya simu tunataka kuondoa cash pay hii itatuwezesha Muhimbili kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha na kuongeza uharaka wa utoaji wa matibabu” amesema