
Kundi la Winnes Crew
Akizungumza na EATV Mwenyekiti wa kundi hilo James Kaligo amesema wameweza kufaidika na Dance100% kwa kuweza kwenda Morogoro, Arusha,na Kilwa ambapo hualikwa kwenda kufanya kazi kwenye matamasha na shughuli nyingine za kijamii kama harusi.
‘’Dance100% imetufanya tutambulike sana kazi zetu na vipaji vyetu vinazidi kung’ara kila siku, tupo watu 7 na moja ya vitu vinavyotufanya tufike mbali ni maelewano ndani ya kundi letu ambapo tukikubaliana kukutana kwenye mazoezi huwa tunajituma sana’’ Amesema James
Kwa upande wake John Joackim amesema wasichana wengi wanashindwa kushiriki katika mashindano hayo kutokana na mazoezi kuwa magumu kutokana na ushindani uliopo.
