Jumanne , 29th Apr , 2014

Chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) kimetoa matokeo ya utafiti unaoonyesha kuwa baadhi ya sheria kandamizi zimechangia kutokuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari hasa kwa idara za serikali kuwa kikwazo cha utoaji taarifa kwa vyombo vya habari.

Baadhi ya wadau wa habari nchini Tanzania wakijadili masuala mbali mbali ya utetezi wa haki ya kupata na kutoa habari

Rais wa TLS Charles Rwechungura, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa matokeo ya utafiti huo ambao umetolewa siku tano kabla ya dunia kuadhimisha Siku ya uhuru wa vyombo vya habari.

Rwechungura akizitaja sheria hizo kuwa ni sheria ya magazeti ya mwaka 2006, sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1970, sheria ya mamlaka ya mawasiliano ya mwaka 2003, sheria ya huduma za polisi na sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na posta ya mwaka 2010.