Jumapili , 3rd Jul , 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu ameungana na viongozi wa dini na wanasiasa katika futari aliyoiandaa jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika futari hiyo Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally amesema kwamba viongozi wa dini waendelee kufundisha masuala ya amani na mshikamano hata baada ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kumalizika.

Kwa upande wake Katibu Kamati ya amani ya viongozi wa dini Padri John Solomon amesema kwamba kitendo cha kushiriki futari pamoja kinaashiria jambo la upendo na mshikamano uliopo nchini.

Aidha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu amewashukuru viongozi wote ambao wamejitokeza na kusema kuwa imekuwa ni jambo la baraka kwake kwa kutoa mwaliko na viongozi hao kuonyesha moyo wa utayari.