Alhamisi , 23rd Jun , 2016

Utafiti mpya uliofanyika nchini Rwanda umebaini kuwa msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi una matokeo mazuri ya kuchumi katika jamii zinazowazunguka, na matokeo yanakuwa bora zaidi pale wakimbizi wanapopewa fedha taslimu badala ya mgao wa chakula.

Moja ya Kambi za Wakimbizi nchini Rwanda

Utafiti huo umefanywa na jopo la watafiti kutoka shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula WFP na chuo kikuu cha California, Davis.

Utafiti ulijikita katika kupima matokeo katika jamii ya msaada wa chakula unaotolewa na WFP kwa wakimbizi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC wanaoishi kwenye kambi tatu nchini Rwanda.

Watafiti wametumia mahojiano ya mamia ya wakimbizi, wanajamii wa Kinyarwanda, na wafanya biashara, na kulinganisha takwimu kati ya wakimbizi makambini wanaopokea fedha taslimu na wanaopokea mgao wa chakula wa kila mwezi.