Jumanne , 21st Jun , 2016

Klabu ya Majimaji imepanga kujiweka sawa kuhakikisha inaongeza mshambuliaji wa kuongeza nguvu ya mashambulizi na Elius Maguli ni kati ya waliomlenga.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Majimaji zinaeleza, tayari wameanza mazungumzo nna Maguli.

“Kweli kuna mazungumzo na Maguri, tunajaribu kuangalia ingawa alitueleza anaweza kucheza nje ya nchi, lakini tunajaribu kuangalia kama inawezekana. Lengo letu ni kuimarisha kikosi,” kilieleza chanzo.

Majimaji chini ya kocha Kally Ongala imefanikiwa kubaki Ligi Kuu Bara na uongozi umesisitiza, msimu ujao unataka kujenga kikosi imara zaidi.