
Ametoa kauli hiyo leo kwenye mahafali ya umoja wa wanachuo ambao ni wanachama wa CHADEMA (CHASO) Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa katiba iliyopo inabana sana kufanya baadhi ya maamuzi huku akitolea mfano tume ya uchaguzi NEC .
Mh. Lowasa amesema kuwa yeye binafsi hakubaliani na utendaji kazi wa tume hiyo hasa pale mgombea uraisi anapokuwa hakubaliani na maamuzi yatakayotangazwa na tume na anashauri ufanyike mchakato wa kuunda chombo kingine kitakachokuwa huru kusimamia shughuli ya uchaguzi.
Katika hatua nyingine Mh Lowasa amezitaja sababu za ujio wa Nabii Joshua nchini Tanzania wakati wa sherehe za kuapishwa kwa Rais wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli kuwa alitumwa kuja kumshawishi akubaliane na matokeo ya uchaguzi lakini alipomueleza ukweli kuhusu uchaguzi huo ndipo mtumishi huyo akaamua kutohudhuria sherehe hizo.